Majaribu Ni Mengi Yanayotujilia


Majaribu ni mengi yanayotujilia.
Bali Mungu anajua yanapotujilia.
Hima atatuongoza mpaka atuitapo.
Tutaelewa vema tufikapo.

(Itikio)
Kutakapopambazuka;
Wateule wakusanyikapo.
Tutahadithia ushindi wetu;
Tutaelewa vema tufikapo.

Mipango yaadimika, nasi twakufamoyo.
Twapotea gizani mioyo ikiwa mizito.
Bali tukiyafuata maneno yake Bwana,
Tutaelewa vema tufikapo.

Majaribu na mitego iliyojificha.
Nayo hutunasa ghafula tusipotarajia.
Basi, twajiuliza, kwani twajaribiwa?
Tutaelewa vema tufikapo.